Mkurugenzi Mkuu kutoka Baraza la Taifa la hifadhi na usimamizi wa Mazingira (NEMC), Dkt. Samuel Gwamaka ametoa onyo kwa wafanyabiashara ambao bado wanaendelea kuingiza nchini vibebeo vilivyopigwa marufuku kwa mujibu wa kanuni ya sheria za mazingira.

Gwamaka amewataka wafanyabiashara kuendelea kubadilisha fikra kwa kuwa mpango uliopo ni kuondoa kabisa malighafi zote zenye madhara.

“Tumekuwa tukitoa maonyo kila mara lakini bado kuna wafanyabiashara wasio waaminifu wanatumia njia za panya kuingiza vibebeo vilivyopigwa marufuku na serikali, kwa sasa tukikukamata tutakufungulia mashitaka na ukibainika kwa mujibu wa sheria za nchi unachukuliwa hatua kali,” amesema Gwamaka.

Aidha, Gwamaka amezitaka halmashauri zote nchini kuhakikisha wanaweka  utaratibu wa kufanya utafiti juu ya aina za taka zinazozalishwa katika maeneo mbalimbali ili iwe  rahisi kuzisafirisha kwenda mahali husika.

Takataka zimetajwa kuwa fursa ambayo jamii inaweza kuitumia kwa kuzikusanya kwa aina ya makundi yake na kuzirejeleza hali inayoweza kuongeza kipato kwa mtu na taifa  kutokana na uwekezaji wa viwanda.

Vichwa vikubwa kuhusishwa na ushirikina
Yaliyowakuta Clouds yahamia Wasafi