Bodi ya Wakurugenzi ya Baraza la Taifa la Hifadhi na usimamizi wa Mazingira (NEMC), imefanya ziara katika mradi wa kuchimba madini aina ya uraniam mkoani Ruvuma utakaoendeshwa na kampuni  ya Mantra Tanzania Limited, kukagua na kujiridhisha hali ya kimazingira ili mradi  utakapoanza usiwe na athari kimazingira hata kijamii bali uwe chachu ya maendeleo katika Taifa letu. 

Mkurugenzi Mkuu wa (NEMC)  Muhandisi Dkt.Samuel Gwamaka amesema kuwa, watu wengi katika jamii wamekuwa na uelewa mdogo juu ya madini ya uraniam  kwani wanaamini kuwa ni madini ambayo yanaathari kubwa katika mazingira na afya za binadamu.

“Tutambue kuwa kila Mradi unapotaka kuanzishwa katika Taifa letu unalazimika kufanyiwa Tathmini ya Athari kwa Mazingira na mradi huu umefanyiwa toka 2012.  Sisi kama Taasisi tumejiridhisha kuwa athari zake ni ndogo. Kimsingi mradi huu ulipewa kibali au cheti cha Tathmini ya Athari kwa Mazingira toka 2012,” Amesema Dkt.Gwamaka.

Kwa upande wake Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi NEMC Dkt.  Catherine Masao amesema kuwa, kama mradi huu utazingatia taratibu walizoeleza na walizopewa na Baraza basi hautakuwa na athari ya kimazingira na kijamii. 

Naye Fredrick Kibodya Mkurugenzi Mtendaji wa  Kampuni ya Mantra Tanzania Limited amesema kuwa, Mradi unafaida kubwa kwa jamii na kitaifa endapo utaanza utasaidia kutoa ajira kwa vijana kwani wanatarajia kuajiri watu wengi sana pamoja na hayo mradi utachangia mapato makubwa ya Taifa.

Azam FC yamsajili Kenneth Muguna
Dkt Mpango kushiriki misa ya kumbukizi ya Hayati Mkapa