Garage kubwa inayotoa huduma ya utengenezaji magari aina mbalimbali iliyopo katika eneo la mtaa wa viwanda Mikocheni jijini Dar es Salaam imefungwa kwa kile kinachodaiwa ni kukiuka sheria ya mazingira na kanuni zake kwa kumwaga mafuta machafu, kutupa vyuma chakavu na kutelekeza magari hovyo yaliyochakaa.

Hatua Hiyo imechukuliwa na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kupitia kwa Mwanasheria wake Mkuu, Vincent Haule, ambapo amesema kuwa Garage hiyo ambayo mmiliki wake hakutambulika mara moja inatakiwa kusimamisha shughuli zote za uendeshaji katika eneo hilo ndani ya siku saba pamoja na kuondoa magari yote.

Aidha, kufuatia kuvunja sheria, taratibu na kanuni za Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC, Garage hiyo imetozwa faini kiasi cha shilingi milioni 10, na kutakiwa kulipa ndani ya wiki mbili.

Kwa upande wake, Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira. Luhaga Mpina amesema kuwa viwanda vinavyochukuliwa hatua kwa uchafuzi wa mazingira vinatakiwa  kutii maagizo ya serikali mara moja.

 

Binti mdogo akutwa kifusini akiwa hai
JPM awaweka mtegoni wawekezaji matapeli