Waziri Mkuu wa Israel, Benjamini Netanyahu amejikuta katika wakati mgumu mara baada ya kukumbwa na tuhuma za ufisadi
Jeshi la Polisi nchini humo limesema kuwa Waziri mkuu Netanyahu anakabiliwa na tuhuma mbalimbali za rushwa na matumizi mabaya ya mali za umma.
Polisi nchini humo imesema kuwa inaushahidi wa kutosha kumtia hatiani Netanyahu kwa tuhuma za rushwa na ufisadi.
Aidha, tuhuma zinazomkabili Netanyahu aliyeongoza nchi hiyo toka mwaka 2009 ni pamoja na ile aliyopokea zawadi ya kiasi cha dola 283,000 kutoka kwa msanii wa Hollywood, Mogul Arnon Milchan na mashabiki wengine, ili kuweza kumsaidia kupata Visa ya marekani.
Hata hivyo, Netanyahu amesema kuwa madai hayo hayana msingi wowote na ataendelea kuwa Waziri mkuu wa nchi hiyo. ingawa wapinzani wanamataka ajiuzulu kwa kupoteza sifa ya kuliongoza taifa hilo.