Makamu wa Rais wa Marekani, Mike Pence amesema kuwa nchi yake itauhamisha Ubalozi wake kutoka Tel Aviv kwenda Jerusalem mwaka 2019.

Amesema kuwa katika kipindi kifupi kijacho utawala wa Rais Trump utafanya mipango ya awali ya kufungua Ubalozi Mjini Jerusalem huku mipango yote ikiendelea kukamilishwa taratibu.

“Jerusalem ni mji mkuu wa Israel, na kama alivyosema, Rais Trump ameielekeza Wizara ya Mambo ya Nje kuanza matayarisho ya awali kuuhamisha ubalozi wetu kutoka Tel Aviv kwenda Jerusalem,”amesema Pence

Aidha, kwa upande wake, Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu amewashukuru Rais Trump na Pence kwa kile alichokiita maamuzi ya kihistoria.

Hata hivyo, Mfalme Abdullah wa Jordan amesema kuwa suluhisho pekee kwa mzozo wa Waisraeli na Wapalestina ni kupatikana kwa suluhisho la muda mrefu la mataifa mawili ambalo limekuwa likizungumziwa na jumuiya ya kimataifa.

 

Diamond afunguka kumiliki kiwanda Rwanda
The Playlist ya Times FM yamtuza Vanessa Mdee ‘Plaque’ ya Nyota wa Mchezo