Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu amezungumza kwa simu na Rais wa Marekani, Joe Biden kwa njia ya simu na kumueleza kuwa anatarajia kuanza upya shughuli zake za mashambulizi huko Gaza kwa nguvu kamili mara baada ya saa za mapatano za kusitisha mapigano kumalizika.
Hatua hiyo ya utulivu uliopo kwasasa inafuatia Israel kusitisha operesheni zake, ili kuruhusu mateka waliokuwa wakizuiliwa katika eneo hilo kuachiliwa na pia wafungwa wa Kipalestina kuruhusiwa kuondoka kutoka magereza ya Israel, ambapo muda wa mapatano hayo unatamatika hii leo.
Netanyahu aanasema atakaribisha kurefushwa kwa mapatano hayo ikiwa itamaanisha kuachiliwa kwa mateka 10 zaidi kila siku, kama ilivyoainishwa katika makubaliano ya awali huku Ikulu ya White House ikisema Viongozi hao wawili Wamekubaliana kuendelea kufanyia kazi suala hilo.
Wizara ya afya ya Gaza inayoongozwa na Hamas, imesema zaidi ya watu 14,500, wakiwemo watoto wasiopungua 5,500, wameuawa huko Gaza tangu Israel ilipoanza kushambulia eneo hilo kwa kulipiza kisasi cha mashambulizi ya Oktoba 7, 2023 huku ikionyesha nia ya kutaka kuzidishwa kwa muda wa kusistisha mapigano.