Klabu ya Middlesbrough iliyorejea ligi kuu ya soka nchini England, inajiandaa kukamilisha mpango wa kumsajili beki kutoka Bosnia na Herzegovina, Neven Subotic.

Kwa mujibu wa gazeti la michezo la nchini Ujerumani (Evening Gazette), beki huyo mwenye umri wa miaka 27, ameshakubali kusaini mkataba wa miaka mitatu baada ya ada yake ya uhamisho ya Pauni milioni 8 kulipwa huko Westfalenstadion.

Subotic ataondoka Borussia Dortmund, alipokua akicheza soka lake kwa miaka minane na anatarajia kuanza changamotoa mpya katika soka la nchini England.

Meneja wa Middlesbrough Aitor Karanka, ameonyesha kujizatiti vilivyo kwa ajili ya msimu ujao wa nchini England, na mpaka sasa ameshakamilisha usajili wa aliyekua mlinda mlango wa FC Barcelona na Man Utd, Victor Valdes.

Gastón Exequiel Ramírez Pereyra

Wakati huo huo Karanka anahusishwa na mipango ya kumalizana na kiungo mshambuliaji kutoka nchini Uruguay, Gastón Exequiel Ramírez Pereyra ambaye kwa sasa yupo huru baada ya mkataba na klabu ya Southampton kufikia tamati.

Ramírez, alicheza kwa mkopo Middlesbrough msimu uliopita na alikua mmoja wa wachezaji waliopambana na kufanikiwa kuirejesha klabu hiyo katika mshike mshike wa ligi kuu nchini England.

Msimu wa 2014-15 Southampton walimtoa kwa mkopo katika klabu ya Hull City.

Mikoa 5 Kupatiwa Huduma za Afya Bure na Madaktari Bigwa Kutoka China
Juventus Waingilia Mpango Wa Babu Wenger