Kiungo wa kati wa Al Hilal, Ruben Neves, amesisitiza kuwa anataka kubaki na timu hiyo ya Saudi Arabia licha ya kutakiwa na Arsenal na Newcastle United zote za England.

Neves, ambaye aliondoka Wolverhampton Wanderers majira ya joto, kuna timu nyingi kwenye Ligi Kuu England zinazomwania kuelekea usajili wa Dirisha Dogo mwezi Januari 2024.

Newcastle awali walionesha nia ya kutaka kumsajili Neves kwa mkopo, lakini sasa wamefikiria kumsajili kiungo huyo wa Al Hilal kwa mkataba wa kudumu.

Arsenal pia ni miongoni mwa timu zinazomfuatilia Neves, lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26, ameweka wazi kuwa hataki kurejea England.

Alipoulizwa kama kuhamia Newcastle Januari 2024 kunawezekana, Neves aliiambia BBC Sport: “Siendi.”

“Nadhani huo ni uvumi kwa sababu ya mmiliki wa klabu na shaka kwa sababu nimecheza England pia.

“Kulikuwa na nia ya Newcastle kabla sijaja hapa, lakini nina furaha sana hapa, familia yangu ina furaha sana, kwa hiyo nina wakati mzuri.

“Kila kitu kinaenda vizuri sana kwangu na ninataka kubaki hapa.”

Al Hilal, inayomilikiwa na Mfuko wa Uwekezaji wa Umma wa Saudia (PIF), ambao wanamiliki Newcastle, walimsajili Neves kwa pauni milioni 47 wakati wa majira ya joto na wamemshuhudia akicheza mechi 19, akiiongoza timu yake kileleni mwa Ligi Kuu ya nchini hiyo.

Kuhamia kwake Mashariki ya Kati kulikuja kwa mshtuko mkubwa kwani Neves mwenye umri wa miaka 26, alikuwa anatakiwa na timu nyingi za Ulaya huku Liverpool na Barcelona wakifuatilia kupatikana kwake kabla ya kiungo huyo kuondoka Molineux.

Xavi: Ninampenda sana Alvaro Morata
Arsenal yakabidhiwa ubingwa England