Notorious B.I.G aliyewahi kulibeba jina la New York begani enzi za uhai wake ikiwa ni miaka 22 ya kifo chake, New York imetoa heshima kubwa kwa B.I.G kwa kuupa jina lake moja ya mtaa jijini humo.
Akizungumza kwenye mahojiano ‘Exclusive’ na mtangazaji wa kituo kimoja cha redio nchini humo, Ebro kwenye kipindi cha In The Morning na mama mzazi wa marehemu B.I.G, Volletta Wallace pamoja na mjukuu wake wamethibitisha kwa kusema mtaa huo “Christopher Wallace Way “utazinduliwa leo tarehe 10 katika makutano ya St James Place &Fulton Street.
Hata hivyo imekuwa destuli kwa jamii kuwapa heshima wasanii wakubwa waliotangulia mbele za haki kwa kuipa majina baadhi ya mitaa yao.
Hivi karibuni rapa Nipsey Hussle aliyepigwa risasi nje ya duka lake la The Marathon Clothes, jina lake lilienziwa na mashabiki wake kwa kulipa jina eneo la makutano ya barabara mjini Los Angeles kupewa jina la Nipsey Hussle kama heshima kwa mchango wake mkubwa kwa jamii.
Eneo St James Place &Fulton Street pataitwa Christopher Wallace Way wakati eneo la Avenue na Crenshaw Blvd limeitwa Nipsey Husssle way ni moja kati ya heshima walizopewa wakali hawa wa Hip Hop kwa michango yao kwenye jamii.