Kocha wa Newcastle United , Eddie Howe, amekiri Klabu hiyo huenda ikasajili wachezaji kutoka Saudi Arabia mwezi Januari 2024, ili kuboresha kikosi chake kilishosheheni wachezaji majeruhi.

Lakini bosi huyo wa Magpies alisema ni “ajabu” Newcastle ndo inatolewa macho zaidi kwenye usajili baada ya klabu za Ligi Kuu England kyinga kupigwa marufuku usajili wa mkopo kutoka Saudi Arabia itakapofika mwzi Januari 2024.

Hiyo inamaanisha Newcastle itakuwa huru kusajili wachezaji kutoka klabu za Saudi Arabia ambayo pia inamilikiwa na Mfuko wa Uwekezaji wa Umma wa Saudi Arabia.

Newcastle inatazamia kufanya usajili wa kiungo wa zamani wa Wolves, Ruben Neves amnbaye amejiunga na Al-Hilal kipindi cha usajili wa kiangazi.

Al-Hilal ni moja ya timu inayosimamiwa na Mfuko wa Uwekezaji wa Umma pamoja na Al-Nassr, Al-Ittihad na Al-Ahli, na wanamiliki mastaa kama Cristiano Ronaldo, NGolo Kante na Riyad Mahrez.

Howe Alisema kuhusu mipango yake Januari: “Newcastle haipo pekee yake, kuna wapinzani, hii sio juu yetu pekee yetu, kila timu ina haki ya kusajili Saudi Arabia, Tunaweza kuruhusiwa kusajili Saudi kama klabu nyingine za Ulaya, sio kama kuna faida, kila klabu zinastahili pia.”

Kutokana na wachezaji wake wengi kuwa majeruhi kocha huyo anataka kulazimisha usajili dirisha dogo kwani kukosekana kwa Sandro Tonali ambaye amefungiwa miezi 10 baada ya kukutwa na hatia ya kucheza kamari, wachezaji kama Sven Botman, Callum Wilson, Harvey Barnes, Dan Burn, Jacob Murphy, Matt Targett na Elliot Anderson wataendelea kuwa nje ya dimba kwa muda mrefu, ingawa Fabian Schar, Miguel Almiron na Alexander Isak wote walitarajiwa kujumuishwa dhidi Chelsea.

Lakini Howe akaongeza: “Hatukuwa na mipango ya kusajili Januari. Lakini itabidi mabosi waliangalie tena hili kwa sababu tuna wachezaji wengi wapo nje wakiuguza majeraha.”

Netanyahu: Muda ukiisha tunashambulia upya
Wakeketaji, wakatili wa kijinsia wakalia kuti kavu