Kampuni ya Saudia Arabia Public Investment Fund chini ya Mfalme Mohammed Bin Salman, ipo tayari kuinunua klabu ya Newcastle United,  kwa kiasi cha Euro milioni 300 kutoka kwa Mike Ashley.

Kampuni hiyo kupitia Mfalme wao Mohammed Bin Salman, imefanya mkutano na Waandishi wa habari na kuweka malengo yake baada ya kuinunua klabu hiyo inayoshiriki ligi kuu ya soka nchini England (EPL).

“Tumefikia pazuri na Mmiliki wa klabu ya Newcastle United wa sasa Mike Ashley, kuwa atatuuzia huku kuna baadhi ya mambo tunaendelea kuweka sawa lengo kubwa kuifanya kuwa timu tishio kwenye ligi kuu England na Barani Ulaya kwa ujumla tunahitaji kushinda taji la UEFA na kusajili mchezaji yoyote kwa gharama yoyote .

“Sisi ni mashabiki wakubwa wa Newcastle United, tulikuwa tunaifuatilia mwendo wake kwenye ligi kuu ya England tunahitaji kuwa tishio kama Chelsea chini ya Roman Abramovich, na Manchester City chini ya Sheikh Mansour na hilo linawezekana, hizi timu mbili zimeleta mapinduzi makubwa kwenye ligi kuu ya England pamoja na Barani Ulaya kwa ujumla.”

“Tuna ndoto za kushinda ligi kuu England pamoja na michuano mikubwa Barani Ulaya na hilo linawezekana mwaka 2019 nilikuwa nataka niinunue klabu ya Manchester United, nilikuwa nipo tayari kuinunua kwa kiasi cha Euro billion 3.8 lakini familia ya Malcom Glazer walikuwa wanataka kiasi cha Euro bilioni 4.9.

“Tunataka kuwasajili wachezaji wakubwa Barani Ulaya, Makocha bora waje kuleta Mapinduzi kwenye timu yetu tunataka tutanue uwanja huo tunaweza tukaendelea kutumia jina la St James Park au kubadilisha jina huu uwanja utakuwa mkubwa na kuingia kwenye miwanja kumi bora duniani kwa ukubwa Mmiliki wa klabu ya Manchester City Sheikh Mansour ni rafiki yangu mkubwa huwa tunaongea sana na nimeona hivi karibuni kashinda mataji, ” Alisema Mohammed Bin Salman.

Endapo mipango ya kampuni ya Saudia Arabia Public Investment Fund chini ya Mfalme Mohammed Bin Salman itafanikiwa na kuinunua klabu ya Newcaste United, itaweka rekodi ya kuwa na uwekezaji mkubwa katika soka la England.

Yondani akingiwa kifua Young Africans
Young Africans wapewa ushauri wa bure