Droo ya Hatua ya 16 Bora ya Champions League imepangwa mchana wa leo ambapo kuan mechi tatu zinazotajwa kuwa zitakuwa na ushindani mkali.

Wababe wa Italia, Juventus wanatarajia kukutana na Tottenham Hotspur katika hatua hiyo mchezo ambao unaaminika utakuwa mgumu huku Real Madrid na  Paris Saint-Germain wakipangwa kukutana, ukiwa ni mchezo mwingine unaoaminika utakuwa na ushindani mkali.

Guzo kubwa ni juu ya  Chelsea wanaonolewa Kocha Antonio Conte ambapo wanatarajiwa kukutana na Barcelona.

Manchester City wao wataanzia ugenini ambapo huko watakipiga dhidi ya Basle wakati Porto wataikaribisha timu nyingine ya England, Liverpool katika hatua hiyo.

Sevilla wao wataanza nyumban I kuikaribisha Manchester United kabla ya timu hizo kurudiana wiki moja baadaye.

Ikumbukwe kuwa michezo ya hatua hiyo itachezwa Februari, mwakani.

Ratiba kamili ya hatua hiyo ni hii hapa:

Juventus vs Tottenham Hotspur

Basle vs Manchester City

Porto vs Liverpool

Sevilla vs Manchester United

Real Madrid vs Paris Saint-Germain

Shakhtar Donetsk vs Roma

Chelsea vs Barcelona

Bayern Munich vs Besiktas

Europa League: Arsenal wapangiwa Ostersunds
LIVE: Miili ya wanajeshi 14 waliouawa DRC ikiwasili Tanzania