Nyota wa timu ya Taifa ya Brazil na klabu ya PSG ya Ufaransa Neymar da Silva Jr amesema kuna tofauti kubwa kati ya wachezaji wa timu ya taifa lake, na wale wanatoka kwenye mataifa ya Afrika, pindi wanapokua kwenye majukumu ya kimataifa.

Neymar ambeya kwa sasa yupo nchini kwao kwa ajili ya ushiriki wa Brazil kwenye Fainali za Mataifa ya Kusini mwa Amerika (Copa Amerika), ametoa dukuduku hilo, kufuatia utofauti unaonekana kwenye kikosi cha mabingwa hao mara tano wa dunia, na timu nyingine duniani, hususan zile za Barani Afrika.

Amesema wachezaji wengi wa Afrika wana vipaji vya hali ya juu, lakini hawajitumi wakiwa katika timu zao za taifa, na matokeo yake hujikuta wanashindwa kuzisaidia timu za mataifa yao, na kuwekeza nguvu nyingi kwenye klabu zao huko Barani Ulaya ama kwingineko duniani.

Pia Neymar ameeleza kuwa wachezaji Waafrika hawana mwamko wa kucheza katika timu zao za taifa kama ilivyokuwa wachezaji wa Amerika ya Kusini

“Wachezaji wengi wa Afrika wana vipaji vya hali ya juu, lakini hawajitumi wakiwa katika timu zao za taifa, hiyo ndiyo tofauti yao na sisi Brazil, ambao kwa sasa tuna makombe matano ya Kombe la Dunia.”

“Waafrika hawana mwamko wa kucheza katika timu zao za taifa kama ilivyo kwa wachezaji wa Amerika ya Kusini, lakini kumbuka wanacheza katika klabu bora za Ulaya na wanaonyesha uwezo wa juu.” ameeleza Nyota huyo wa Brazil NeymarJr.

Asimilia kubwa ya wachezaji wa Afrika wamekua kwenye malumbano na mashabiki wa mataifa yao, kufuatia kuonesha viwango duni wanapokua kwenye jukumu la kuzutumikia timu zao za taifa, wakilinganishwa na wanapokua kwenye majukumu yao mengine ndani ya uwanja kwenye klabu zao.

Copa America 2021: Brazil yatangulia Robo Fainali
Matty Mseti: Sina sababu ya kuondoka Simba