Nyota wa Al Hilal Neymar amesema Ligi ya Saudi Arabia itakuwa na nguvu zaidi kuliko Ligue l baada ya kufuatia uhamisho wake wa Pauni 77.5 milioni.

Nahodha huyo wa Timu ya Taifa ya Brazil alihamia Saudi akitokea Paris St-Germain kweye dirisha la usajili la kiangazi mwezi uliopita.

Neymar alitua Al-Hi-lal ikishuhudiwa timu za Kiarabu zikitumia Pauni 700 milioni kwenye usajili wa wachezaji kutoka Ulaya.

Akizungumza na waandishi wa habari Neymar alisema: ” Majina makubwa ya wachezaji yamejiunga na ligi ya Saudia, sitashangaa kuona ligi hiyo ikiwa bora zaidi ya Ligue l siku za usoni.”

Neymar aligoma kuendelea kukipiga PSG baada ya Lionel Messi kujiunga na Inter Miami inayomilikiwa na David Beckham, lakini sasa anafurahia maisha Uarabuni akiwa na Al-Hilal.

El- Ettifaq ilimsajili Georginio Wijnaldum mchezaji mwenzake wa zamani Neymar kutoka PSG, huku Mastaa wengine kama Karim Benzema na Sadio Mane wakitimkia huko.

Mwingine ni nahodha wa zamani wa Inter Milan, Marcelo Brozovic, beki wa Barcelona Franck Kessie, Jota na kiungo wa Lazio Sergej Milinkovic-Savic.

Kungekuwa na rekodi ya usajili ya dunia endapo Al-Hilal ingepewa ruhusa ya kuongea na Kylian Mbappe baada ya kuweka mezani ofa ya Pauni 259 milioni, lakini Mshambuliaji huyo wa P’SG aligoma na kubaki na mabingwa hao wa Ufaransa badala yake Neymar akanunuliwa.

Ahmed Ally afichua ramani ya Kimataifa
Diaspora wamlilia Kairuki, waahidi ushirikiano kwa Balozi Khamis