Nahodha na mashambuliaji wa timu ya taifa ya Brazil, Neymar da Silva Santos Júnior, amempigia chapuo rafiki yake kipenzi Philippe Coutinho kwa kusema anatosha kuwa sehemu ya kikosi cha FC Barcelona.

Naymar amezungumza jambo hilo huku ulimwengu ukifahamu ana urafiki mkubwa na Coutinho tangu walipokua na umri mdogo, na huenda kauli yake ikachukuliwa kama anataka kuwa karibu na mchezaji huyo wa klabu ya Liverpool.

Neymar amesema Coutinho ana vigezo vyote vya kuitumikia FC Barcelona na angependezwa siku moja awe sehemu ya kikosi cha klabu hiyo ambayo imekua na mvuto kwa wachezaji wengi duniani kutokana na soka linalochezwa klabuni hapo.

Amesema amekua akimfuatilia kiungo huyo mshambuliaji na amebaini ana kitu tofauti na wachezaji wengine, na ana kipaji cha kipekee ambacho kitaendelea kuisaidia klabu yake ya Liverpool anayoitumikia kwa sasa, hivyo anaamini kama angelikua FC Barcelona angelionekana zaidi na ulimwengu ungeelewa nini anachokizungumza kwa sasa.

Philippe Coutinho alisajiliwa na Liverpool mwaka 2013 akitokea Inter Milan nchini Italia na mpaka sasa amekua tegemeo kubwa huko Anfield kutokana na uwezo na ushirikiano anaouonyesha dhidi ya wachezaji wenzake huko Anfield.

Mpaka sasa Philippe Coutinho ameshaichezea Liverpool katika michezo 85 na kufunga mabao 14.

Utafiti Wa 'TWAWEZA' Wampa Magufuli Ushindi Wa Kishindo Dhidi Ya Lowassa
CCM: Waompenda Lowassa Wavue Magwanda