Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Brazil, Carlos Dunga ametaja kikosi  kitakachoanza kampeni ya kusaka nafasi ya kucheza fainali za kombe la dunia za mwaka 2018 dhidi ya Chile pamoja na Venezuela mapema mwezi ujao.

Dunga ametaja kikosi chake kwa kumuengua nahodha na mshambuliaji wa mabingwa hao wa kihistoria duniani, Neymar da Silva Santos Júnior kufuatia adhabu ya kufungiwa michezo minne iliyotolewa shirikisho la soka la Amerika ya kusini CAMNEBOL wakati wa fainali za mataifa ya ukanda huo zilizochezwa miezi mitau iliyopita.

Kikosi kamili kilichotajwa na Carlos Dunga tayari kwa mpambano ya kuelekea nchini Urusi kusaka ubingwa wa dunia mwaka 2018, upande wa makipa ni Jefferson (Botafogo), Marcelo Grohe (Grêmio) na Alisson (Internacional)

Mabeki ni Rafinha (Bayern Munich), Marcelo (Real Madrid), Filipe Luis (Atlético de Madrid), Fabinho (Monaco), David Luiz (PSG), Miranda (Inter de Milão), Marquinhos (PSG), Gil (Corinthians)

Viungo: Luiz Gustavo (Wolfsburg), Fernandinho (Manchester City), Elias (Corinthians), Renato Augusto (Corinthians), Lucas Lima (Santos), Lucas Moura (PSG), Willian (Chelsea)

Washambuliaji: Douglas Costa (Bayern), Philippe Coutinho (Liverpool), Oscar (Chelsea), Roberto Firmino (Liverpool), Hulk (Zenit)

Brazil wataanza kupambana na Chile mjini Santiago kwenye uwanja wa Nacional Julio Martínez Prádanos, oktoba 8 na kisha watarejea nyumbani kuchezana Venezuela oktoba 13 kwenye uwanja wa Castelão, uliopo mjini Fortaleza.

H Baba Ampa Mwanae Zawadi Ya Kiutuuzima
Man Utd Waanguka Tena Kimapato