Mshambuliaji wa Al-Hilal Neymar atakuwa nje ya dimba msimu mzima baada ya kuumia goti katika mechi ya kufuzu Kombe la Dunia 2026 Brazil ilipomenyana dhidi ya Uruguay.

Mshambuliaji huyo aliumia vibaya goti wakati wa mechi ya kufuzu Kombe la Dunia (2026) dhidi ya Uruguay kufuatia kichapo cha mabao 2-0 na huenda akakaa nje kwa muda mrefu.

Neymar aliumia vibaya wakati anajaribu kumpokonya mpira mchezaji wa Uruguay, Nicolas de la Cruz lakini akajikuta amepigiza goti chini.

Wachezaji wenzake wa Brazil walihamaki baada ya tukio hilo na kumzunguka wakati amelala chini akiwa anaugulia maumivu makali.

Kwa mujibu wa taarifa Neymar alilazimika kufanyiwa upasuaji haraka kutibu jeraha hilo la goti sasa atakuwa nje kwa muda mrefu.

Wakati huo huo mashabiki wa soka wamechukizwa na kitendo cha Klabu ya Al-Hilal kuweka picha ya Neymar aliyoumia mtandaoni wakimtakia kila la kheri apone haraka.

Shabiki mmoja akakomenti kwenye picha hiyo akisema: “Nataka kujua nani ameruhusu picha ya Neymar kuwekwa mtandaoni?”

Mwingine akaandika: “Huu ni mtandao mbovu wa kijamii katika historia ya soka Nani alifikiria hivyo?.”

Shabiki mwingine akaandika kwa hasira: “Mjinga gani amefanya uamuzi picha yake ya kuumia itumike?

Mchezaji huyo ghali zaidi katika historia soka ambaye aligharimu Pauni 196 milioni alipojiunga na Paris Saint-Germain mwaka 2017 alifanyiwa vipimo ili kubaini ukubwa wa jeraha lake.

Nayo klabu yake ya sasa Al Hilal ilifichua kuwa Neymar ameumia vibaya huku kukiwa na haja ya kufanyiwa upasuaji kwenye goti lake.

Kakolanya atoa neno la shukurani Singida BS
Simba yaahidi makubwa African Football League