Mshambuliaji Neymar Jr ameendelea kuwa moto wa kuotea mbali katika ligi ya Ufaransa, baada ya kuifungia Paris Saint Germain (PSG), bao la ushindi katika mchezo dhidi ya Olympic Lyon.

Neymar ambaye alipoteza imani dhidi ya mashabiki wa PSG kufuatia sakata lake la kutaka kuondoka wakati wa usajili wa majira ya kiangazi, aliiwezesha timu yake kuibuka na ushindi huo, ikicheza ugenini jana jumapili.

Neymar alifunga bao kwa kiki ya mguu wa kushoto zikiwa zimebaki dakika tatu kabla ya mpira kumalizika.

Hii ni mara ya pili kwa mshambuliaji huyo kutoka nchini Brazil kuifungia bao muhimu PSG, kwani alifanya hivyo katika mchezo uliopita dhidi ya Strasbourg.

Neymar amerejea katika ubora wake baada ya kukosa michezo mitano tano tangu alipoibua mjadala wa kutaka kurejea FC Barcelona katika usajili wa majira ya kiangazi kabla ya mpango huo kukwama.

Wanafunzi 7 wafariki papo hapo kwa 'kuporomokewa' na paa
Mbaroni kwa kusafirisha viroba vya madini bila kibali.