FC Barcelona wameanza mpango wa kufanya mazungumzo ya kumsainisha mkataba mpya mshambuliaji Neymar Da Silva Santos Junior ambaye siku mbili zilizopita alihusishwa na mipango ya kutaka kusajiliwa na Man Utd.

Taratibu za mazungumzo kati ya viongozi na mshambuliaji huyo zinakwenda vizuri huku rais wa FC Barcelona Josep Bartomeu, akionyesha Imani kubwa wa jambo hilo kukamilishwa mwaka huu.

Inahisiwa kwamba FC Barcelona itawagharimu kiasi cha paund million 182, kukamilisha mpango wa kumsainisha mkataba mpya Neymar ambaye kwa sasa ana muda wa miaka miwili tangu aliposajiliwa mwaka 2013 akitokea nchini kwao Brazil alipokua akiitumikia klabu ya Santos.

Mkataba wa sasa wa Neymar, unatarajia kufikia kikomo mwaka 2018, lakini kinachofanywa na viongozi wa Fc Barcelona ni kutengeneza mazingira ya kuzikatisha tamaa klabu nyingine ambazo zitakuwa tayari kumsajili mshambuliaji huyo.

Twiga Yajifua Zanzibar
U-15 Yajifua Morogoro