Dirisha la usajili barani Ulaya limefungwa mpaka ifikapo mwezi Januari lakini haizuii kuwepo kwa mazungumzo ya kufikia makubaliano ya kununua wachezaji na minong’ong’ono ya usajili tayari imeanza katika vyombo mbali vya habari duniani.

Gazeti la ‘Mundo Deportivo’ ambalo huandika habari za michezo nchini Hispania limeripoti kuwa klabu ya Real Madrid inataka kumsajili mshambuliaji wa Paris Saint-Germain, Neymar ili awe mrithi wa muda mrefu wa Cristiano Ronaldo.

Neymar alijiunga na Paris Saint-Germain kwa ada iliyoweka rekodi ya dunia ya Pauni milioni 198 lakini Madrid ambao walishataka kumshaji haka kabla hajasajiliwa na Barcelona mwaka 2013 bado wanaonyesha nia ya kumtaka mbrazili huyo.

Hakuna dalili zozote kwamba Neymar hana furaha ndani ya PSG lakini Madrid wanatamani kumuona Neymar akitua Santiago Bernabeu jambo ambalo huenda likawa gumu kwani PSG watafanya kila linalowezeka kumtuliza Neymar asahau habari za Madrid.

Kesi mbili za kupinga matokeo zafunguliwa Kenya
Lowassa, Nyalandu waanza kupanga mikakati ya 2020