Waziri wa Zamani wa Nishati na Madini na Mbunge wa Jimbo la Sengerema, William Ngeleja amekiri kuchukua mgao wa shilingi milioni 40.4 kutoka kwa Kampuni ya James Rugemalira ya Engineering Marketing kupitia Benki ya Mkombozi.
Ngeleja amewasilisha kiasi hicho cha fedha hizo Serikalini ili kuweza kuepukana na kuandamwa mara kwa mara katika sakata hilo ambalo limekuwa likichukua sura mpya kila kukicha baada ya mmiliki wa Kampuni hiyo kukamatwa na Jeshi la Polisi.
“Nakiri kupokea fedha hizo kama msaada kutoka kwa ndugu Rugemalira ili zinisaidie katika kutimiza majukumu yangu hususani katika jimbo langu la Sengerema, hivyo nimeamua kuzirudisha kwa sababu nilizipata fedha hizo bila kujua kama zina kashifa ya Escrowa,”amesema Ngeleja.
-
Ripoti ya PAC yaanika vigogo, wanasiasa na viongozi wa dini upigaji hela za Escrow
-
Mikataba ya Madini pasua kichwa, Serikali yasema haitavunjwa
-
JPM: Sisafiri sasa hivi, lazima niwanyooshe kwanza, hizi safari zipo tu
Aidha, amesema kuwa kwa mujibu wa Sheria ya Maadili ya Umma namba 13 ya mwaka 1995, ameamua kurudisha msaada huo Serikalini (TRA) kwa hiari bila kujali kama alishalipia kodi Serikalini.
Hata hivyo, Ngeleja ameongeza kuwa kupokea msaada sio kosa lakini pindi inapobainika kuwa msaada huo sio halali ni vyema ukarudishwa sehemu husika, pia amempongeza na kumuunga mkono Rais Dkt. Magufuli kwa kazi kubwa anayoifanya ya kutetea rasilimali za taifa.