Katibu wa NEC ya CCM, Siasa na Mahusiano ya Kimataifa, Ngemela Lubinga amesema kuwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 ulikuwa mgumu kutokana na wanachama wa chama hicho kutokuwa wasiri.

Amesema kuwa umakini wa kutekeleza majukumu na umakini wa kutunza siri za chama kwa baadhi ya wanachama wa chama hicho ulikuwa ni mdogo hivyo kusababisha kuvuja kwa baadhi ya siri kitu ambacho kilisababisha chama kuyumba.

Ameyasema hayo hii leo jijini Dar es salaam kwenye mkutano wa baraza la jumuiya ya wazazi CCM Taifa, ambapo amesema kuwa kutunza siri kutawaongezea heshima wanachama katika jamii.

“Ilikuwa ni miaka ya misukosuko, tumepita katika mabonde na milima, lakini leo tunatembea kifua mbele, lakini niwakumbushe kwamba hakuna mfumo wowote duniani usiojengwa kwa usiri,”amesema Lubinga

Hata hivyo, Takribani nusu ya wajumbe wa baraza hilo linalokutana kupitia majina ya walioomba kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika jumuiya hiyo walitoka ndani ya ukumbi huo kutokana na kuomba tena nafasi za kugombea.

Moze Iyobo kafanya makubwa kumbadilisha Aunty Ezekiel
Azam yajinoa vikali kuikabili Mbao Fc