Kiungo wa klabu bingwa nchini England Chelsea N’Golo Kante, ameondolewa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Ufaransa, ipo katika maandalizi ya mwisho ya kujiandaa na mchezo wa kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia dhidi ya Belarus, utakaochezwa kesho jijini Paris.

Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Ufaransa Didier Deschamps, amethibitisha kuondoka kwa kiungo huyo katika kambi ya kikosi chake, kufuatia maumivu ya misuli ambayo aliyapata mwishoni mwa juma lililopita wakati wa mchezo dhidi ya Bulgaria.

Deschamps amesema Kante amefanyia vipimo na imebainika hatoweza kuwa sehemu ya kikosi chake katika mchezo wa kesho, na sasa analazimika kurejea jijini London kwa ajili ya kupatiwa matibabu na madaktari wa klabu ya Chelsea.

Katika mchezo dhidi ya Bulgaria, Kante alicheza kwa dakika 30 na alilazimika kutolewa nje ya uwanja, baada ya kupata majeraha ya misuli ya paja na nafasi yake kuchukuliwa na kiungo Adrien Rabiot.

Timu ya taifa ya Ufaransa (Les Bleus) inaongoza msimamo wa kundi A kwa kuwa na point 20, na wanahitaji point tatu ili kujihakikishia nafasi ya kucheza fainali za kombe la dunia.

Ufaransa inaongoza msimamo wa kundi A kwa tofauti ya pointi moja mbele ya Sweden.

Rammy Galis kutoka na Aki na Ukwa wa Nigeria
Wanaowania tuzo ya Ballon d'Or waanza kutajwa