Timu ya taifa ya Tanzania, chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes), kesho Alhamis itarejea dimbani kucheza mchezo wa pili wa kundi ‘A’ dhidi ya Somalia, kwenye michuano ya vijana ya Afrika Mashariki na Kati (CECAFA U20) inayoendelea mkoani Arusha.

Tanzania ilianza vyema michuano hiyo katika kituo cha Karatu (Uwanja wa Black Rhimo) kwa kuichapa Djibouti mabao sita kwa moja, na kuongoza msimamo wa kundi A.

Kocha mkuu wa Ngorongoro Heroes Jamhuri Kihwelo, ‘Julio’ amesema ana imani na kikosi chake kufanya vizuri katika mchezo huo, ambao utaamua utakua wa mwisho kwa kundi hilo, ambalo lina timu tatu.

Amesema amewafuatilia Somalia kupitia mchezo wa jana dhidi ya Djibouti, na kubaini ubora na mapungufu yao kabla ya kukutana nao kesho Alhamis, Novemba 26.

“Baada ya ushindi mnono dhidi ya Djibout, matokeo hayo hayatufanyi kujiamini zaidi na kutoendelea kujifua kwa kufanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza katika mchezo uliopita,” amesema Julio ambaye kikosi chake kiliibuka na ushindi wa mabao 6-1 dhidi ya Djibouti.

Nchi zinazoshiriki michuano hiyo ni mwenyeji Tanzania, Kenya, Sudan, Uganda, Sudan Kusini, Somalia, Djibouti, Ethiopia na Burundi.

Cioaba: Tupo tayari kuikabili Young Africans
Halima Mdee na wenzake kikaangoni CHADEMA

Comments

comments