Serikali inaendelea kuongeza nguvu ya uzalishashi katika Kilimo, Mifugo, uvuvi na vyuma ili kukabili changamoto ya upungufu malighafi inayokabili viwanda vingi nchini na kusababisha viwanda hivyo kuzalisha chini ya uwezo na kiwango cha uzalishaji.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo alipotembelea kiwanda cha OK Plast Ltd kinachozalisha bidhaa za nyaya za umeme Pamoja na mikeka na kukuta kuna changamoto ya upungufu wa malighafi ya mabaki ya shaba kwa ajiri ya kiwanda hicho.
“Nikili kwamba moja ya changamoto kubwa katika viwanda vya Tanzania kwa sasa ni malighafi sio idadi ya viwanda, idadi ya viwanda ipo ya kutosha lakini viwanda vyetu vingi vinazalisha chini ya uwezo kwa sababu ya kukosekana kwa malighafi kwahiyo tuna kazi kubwa ya kuongeza uzalishaji katika kilimo, mifugo, uvuvi na vyuma,” Amesema Prof. Mkumbo
Aidha, Waziri Mkumbo ameaihidi kukutana na Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais – Muungano na Mazingira, Suleiman Jafo, ili kujadili na kuona namna ya kusaidia kiwanda hicho na viwanda vingine vyenye changamoto ya malighafi ya mabaki ya shaba na chuma ili kuona namna ya kusaidia mabaki hayo kuuzwa kwa viwanda vya ndani kuliko kusafilishwa kwenda nje.
Sambamba na hayo Waziri Mkumbo amewahasa watanzania kununua bidhaa zilizozalishwa nchini na zilizodhibitishwa na Shirika la Viwango Tanzania maana kwa sasa viwanda vya ndani vinazalisha bidhaa bora na zenye viwango.
Naye Mkuu wa Idara ya Sheria na Uzingatiaji Sheria wa Kiwanda cha OK Plast Ltd, Bw. Anackreto Pereilla ameishukuru Serikali kuwa kusikiza Changamoto yao ya upungufu wa malighafi ambayo imekuwa adimu kutokana na malighafi hiyo kusafirishwa kwenda nje.