Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI, Stanslaus Nyongo ameutaka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya – NHIF, kuongeza kasi na Ufanisi wa utoaji elimu kwa Wananchi ili kuboresha utoaji wa huduma bora za afya nchini.

Nyongo ameyasema hayo na kuongeza kuwa, utoaji wa elimu kwa wananchi kuhusu huduma za Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya itapunguza malalamiko kwa wananchi ambao hawakua na uelewa kuhusiana na huduma za Mfuko huo.

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Bima ya Afya – NHIF, Bernard Konga amesema Katika kipindi cha kuanzia Julai 2022 hadi Juni 2023 mfuko kupitia Kitengo cha Kudhibiti na kupambana na udanganyifu, uliweza kubaini madai yasiyo halali ya shilingi bilioni 7.26 kutoka kwa watoa huduma mbalimbali.

Kwa upande wake Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesisitiza kuchukuliwa hatua kwa vituo na Wanachama wadanganyifu ili mfuko huo uweze kutoa huduma bora na za kiuhalali kwa wanachama, huku akiutaka Mfuko huo kuongeza wanachama ili mfuko uweze kukua na kuendelea kutoa huduma bora kwa wanachama wa NHIF.

Rejesheni fedha za kigeni kuimarisha uchumi - Biteko
Karim Mandonga yupo huru, kuzichapa Znz