Kufuatia zoezi linaloendelea jijini Dar es salam lililoanzishwa na Mkuu wa Mkoa huo, Paul Makonda la kushughulikia na kuwasaidia kisheria wanawake wote waliotelekezwa na waume zao mara baada ya kuzalishwa, mdau mmoja amejitokeza na kujitolea Shilingi Milioni 250.
Kufuatia pesa hiyo Makonda ametangaza neema kwa watoto hao ambapo watapatiwa bima ya Afya kwa mwaka mzima kwa ajili ya matibabu.
Zoezi la utoaji wa huduma hiyo tayari limekwishaanza, ambapo Meneja kutoka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya NHIF, kanda ya Ilala Happyness Sima amesema wamejipanga kuandikisha watoto wasiopungua 1,000 kwa siku.
Hivyo amewaasa wakinamama hao kuhakikisha wanakuja na nyaraka zote zinazohitajika kuambatanisha katika fomu ya kuomba bima, ametaja viambatanisho hivyo kuwa ni Cheti cha Kuzaliwa pamoja na picha ya mtoto.
-
Video: Sakata la Makonda laanza kuzaa matunda, mmoja akamatwa
-
mnywesha sumu mwanae kunusuru ndoa yake
Aidha Makonda amesema hadi jana tayari wakinamama 1,498 tayari wameshasikilizwa na wanasheria.
Shirika la Taifa la Bima ya Afya, NHIF, linatoa huduma za bima ya Afya kwa gharama nafuu kabisa, kwa watoto chini ya miaka 18, kupitia bima yao ya ”Toto Afya” ambapo mtoto anapata matibabu ya mwaka mzima kwa gharama za shilingi 50,400 tu, hivyo wazazi ambao hawajatelekezwa pia wana nafasi ya kujipatia bima ya Afya ili kumuhakikishia mtoto matibabu ya mwaka mzima.