Kipre Bolou bado anaumwa kisigino na kwa mara nyingine tena ataukosa mchezo wa kesho dhidi ya Yanga. Lakini Azam FC ina wachezaji bora wengi kwenye eneo la kiungo kucheza badala yake.

Jean Baptiste Mugiraneza Migi, Himid Mao Mkami, Salum Abubakar Sureboy, Mudathir Yahya Abbas na Frank Domayo ni baadhi ya majina makubwa nchini ya viungo wanaotarajiwa kutetea jahazi la Azam FC hapo kesho.

Utamu wa mechi ya kesho ni kwamba itakuwa mechi ya kisasi kwa timu mbili ambazo zamani kidogo mashabiki wake walikuwa hasimu, lakini siku za karibuni wameonekana kuweka pembeni uhasimu wa chuki na kufanya uhasimu wa ushabiki wa utani wa kimichezo.

Historia inaonesha uhasimu wa Azam FC na Yanga ulitokana na Azam FC kumsajili mchezaji kipenzi cha Yanga Mrisho Ngasa na baadaye kuitandika Yanga Mabao 4-1 machi ambayo wachezaji wa Yanga walishindwa kuzuia mihemuko na hasira zao uwanjani hivyo kufanya fujo zilizopelekea baadhi yao kupewa kadi nyekundu na mwamuzi na baadaye mashabiki wao kulalamika kuwa kadi zile hazikuwa halali hivyo mwamuzi Israel Nkongo aliwadhulumu.

Lakini baada ya misimu kadhaa kupita, inaonekana tofauti hizo zimewekwa kando. Mashabiki na viongozi wa Azam FC na Yanga wanaheshimiana sana. Azam FC inajua uwezo wa Yanga kisoka na kimkakati na kuiheshimu kama klabu kubwa nchini lakini pia Yanga wanaheshimu vipaji vilivyopo Azam FC ambapo bila shaka ndicho kikosi bora zaidi kwa sasa.

Mechi ya kesho inatarajiwa kuwa na ufundi mkubwa, Kocha wa Yanga Hans Van De Plujm anajulikana kupenda kucheza soka la kukaba pamoja na kushabulia muda wote. Yanga ina washambuliaji wenye kasi na vipaji kama Mwaishuya, kaseke, Msuva, Tambwe na Ngoma. Hawa watakutana na ukuta wa chuma wa Stewart Hall unaoongozwa na Serge Wawa Pascal, Aggrey Morris, Said Moradi, Erasto Nyoni na Shamari Kapombe.

Itakuwa mechi ya kusisimua kwani washambuliaji wa Azam FC wakiongozwa na nahodha John Raphael Bocco na Kipre Tchetche wanajulikana kwa ubora wao nasafari hii wamerejesha makali yao.

Timu zote mbili zimefanya maandalizi ya nguvu. Azam FC wakitokea kisiwani Zanzibar huku Yanga wakirejea toka mkoani Mbeya walikoweka kambi.

Tusubiri dakika 90 za mchezo

Buffon Awakumbuka Vidal, Tevez Na Andrea Pirlo
Polisi: Marufuku Kuwazomea Waliovaa Sare Za Chama