Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuwa kama viongozi wameshindwa kusimamia migodi ni bora kuifunga ili waje kusimamia kizazi kijacho kuliko kuendelea kuhujumu uchumi na rasilimali za nchi.

Ameyasema hayo Ikulu jijini Dar es salaam mara baada kukabidhiwa ripoti za uchunguzi wa madini uliofanywa na kamati mbili za bunge, ambapo amesema kuwa nchi hii haikutakiwa kuwa hapa ilipo kiuchumi.

Aidha, amesema kuwa ni bora kuanza moja kwenye kusimamia rasilimali za taifa kuliko kuacha ziendelee kuhujumiwa na watu ambao hawana faida yeyote katika nchi ya Tanzania.

“Ni mara kumi haya madini yasiuzwe ili kizazi kijacho kiyakute, kama madini haya tumeibiwa tufunge watakuja watoto wetu watachimba, nataka tufike mahali kama ni kuanza upya tuanze upya,”amesema Rais Dkt. Magufuli

Hata hivyo, ripoti ya uchunguzi wa madini imekabidhiwa jana kwa Rais Magufuli na kusema kuwa ataitolea uamuzi siku chache zijazo, huku akiwataka wahusika waliotajwa kwenye ripoti hiyo waliochagia kuhujumu uchumi kujiuzulu nyadhifa.

 

Fahamu chimbuko la wanawake kuvaa wigi
Video: Ndugai atoa ufafanuzi kuhusu matibabu ya Lissu