TP Mazembe itamenyana na El Merreikh ya Sudan katika Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, mchezo wa kwanza ukichezwa Septemba 25, mwaka huu mjini Khartoum na marudiano Oktoba 2 mjini Lubumbashi.

Huo ni mtihani mkubwa kwa Mazembe, kwani imekuwa ikisumbuliwa mno na timu za Sudan- katika hatua ya makundi mwaka huu ilipangwa na El Hilal na haikushinda hata mchezo mmoja.

Mchezo wa kwanza Lubumbashi ililazimishwa sare kabla ya kufungwa 1-0 mchezo wa marudiano Sudan- na saa wanakutana na timu ambayo inaaminika ndiyo bora zaidi nchini humo.

Nusu Fainali nyingine ya Ligi ya Mabingwa Afrika itakuwa kati ya El Hilal ya Sudan na USM Alger ya Algeria, nao pia mechi ya kwanza itakuwa Septemba 25 na marudiano Oktoba 2, mwaka huu.

Rais wa TP Mazembe, Moise Katumbi Chapwe amefurahia ushindi wa 5-0 katika mchezo wa mwisho mwishoni mwa wiki dhidi ya Moghreb Tetouan YA Morocco na kuongoza Kundi A, Mbwana Ally Samatta wa Tanzania akifunga mabao matatu.

“Kabla ya mchezo, nilitarajia mabao mawili kwa Mbwana Samatta. Ni mchezaji babu kubwa ambaye aliibuka baada ya kipindi kigumu alichopitia. Wakati wote nawaamini wachezaji, kwa sababu kuna wakati wanakuwa hawajisikii vizuri. Mbwana Samatta amefunga, tunatarajia kufanya vizuri zaidi,”amesema katumbi.

Ikumbukwe, safari ya Merreikh katika Ligi ya Mabingwa Afrika ilianzia Dar es Salaam ambako ilifungwa 2-0 na Azam FC, kabla ya kwenda kushinda 3-0 nyumbani katika mchezo wa marudiano na kusonga mbele.

NUSU FAINALI LIGI YA MABINGWA:
Septemba 25, 2015
El Merreikh Vs TP Mazembe
El Hilal Vs USM Alger
Oktoba 2, 2015
TP Mazembe Vs El Merreikh
USM Alger Vs El Hilal

Man Utd Wapata Pigo Kubwa Ugenini
Mbatia: Tunataka Mdahalo Na CCM, Lowassa Hakuomba Kura Kanisani