Hivi ni kweli Shatta Wale kafariki Dunia? Hilo ni miongoni mwa maswali ambayo mashabiki wa Mwanamuziki kutoka nchini Ghana Charles Nii Armah Mensah Jr, maarufuShatta Wale wamekuwa wakijiuliza kwa siku mbili mfululizo kufuatia uvumi wa taarifa za msanii huyo kufariki kwa kupigwa risasi suku ya Jumatatu octoba 18,2021.
Kufuatia sintofahamu hiyo Jeshi la Polisi nchini Ghana limeibuka na taarifa ya uamuzi wa kufanya uchunguzi juu ya taarifa hizo zinzoendelea kusambaa kwa kazi sehemu mbali mbali ikiwamo kwenye mitandao ya kijamii.
Taarifa za kupigwa risasi na kuuawa kwa msanii huyo zilianza kuenea kwa kasi siku ya Juamatatu, baada ya msaidizi wa Shatta Wale aitwaye Nana Dope kutoa taarifa zilizohusisha vurugu zilizosababisha vita ya risasi iliyopelekea kujeruhiwa vibaya kwa Mwanamuziki Shatta Wale na kukimbizwa hospital akiwa na hali mbaya sana.
Hofu kubwa kwa watu wengi nchini Ghana inakuja kufuatia utabiri uliotole mapema Septemba 28, 2021 na Askofu maarufu Stephen Akwasi (Jesus Ahoufe) aliyewahi kusema wazi kuwa kifo cha Msanii Shatta wale kitatokana na kushambuliwa kwa risasi siku na tarehe kama ya jana jumatatu, yaani tarehe 8 oktoba 2021.
Japo hakufafanua kwa undani lakini aliweka wazi kuwa kikosi cha watu wenye silaha kitakuwa chanzo cha kifo chake na kutoa rai kwa msanii huyo kuwahi kumtafuta ili amuombee ili kumuepusha na janga hilo mbele yake.
Siku chache kupitia ukurasa wake wa mtandao wa facebook Shatta wale aliandika maneno yenye kusomeka “maisha yangu yako hatarini na ninaendelea kukimbia mpaka nchi itakapo nionyesha sheria.” Ambapo aliongeza kwa kusema pengine aina ya utabiri wenye kutolewa hadharani na watumishi wa Mungu ukawa chachu ya maadui kuibuka na kuamua kumpiga risasi kweli kweli kwa sababu binafsi kupitia maneno yaliyotolewa na Askofu Akwasi.