Mapema mwaka huu wa 2023, Waziri wa Maendeleo ya Jami, Jinsia na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima aliwahi kusema Serikali ya awamu ya sita imewainua Wanawake kiuchumi kwa kuwapatia fursa za kiteknolojia na mikopo yenye masharti nafuu, ili waweze kupambana na ukatili wa kijinsia.

Dkt. Gwajima, aliyasema haya wakati wa Mkutano Mkuu wa Tano wa Mwanamke kiongozi kwa mwaka z023, uliofanyika jijini Dar es Salaam.

“Serikali ya awamu ya sita imewainua wanawake kiuchumi kwa kuwapatia fursa za kiteknolojia na mikopo yenye masharti nafuu ili waweze kupambana na ukatili wa kijinsia,” alisema Waziri Dkt. Gwajima.

Aidha, alizidi kubainisha kwamba, Serikali pia imeratibu programu ya kuwezesha Wanawake katika maendeleo na mwelekeo wa kidijitali, ili wafahamu masuala ya sayansi, teknolojia, uhandisi na hesabu.

Kwa lugha nyepesi na isiyo na mawaa ni kweli Wanawake wameinuka kiuchumi, kwani sehemu kubwa ya jinsia hiyo, kwasasa inaongoza kwa tabasamu hapa nchini.

Baadhi ya Watu wanadai ukitaka kuangalia iwapo wameinuka kiuchumu, ni rahisi kugundua, yaani kaa barabarani halafu angalia magari yanayopita uone yanaendeshwa na akina nani kama si akina mama kwa wingi. Kwako binafsi unalionaje hili?

 

Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Desemba 21, 2023
Busu, kumbatio vyatajwa kuwa hatari kwa afya