Meneja mpya klabu ya Man City Pep Guardiola, amepiga marufuku ulaji wa vyakula vya kupikwa kwa haraka na vile vinavyopikwa kwa mafuta mengi.

Beki wa pembeni wa klabu hiyo Gael Clichy, amewaambia waandishi wa habari kuwa meneja huyo kutoka nchini Hispania, amepiga marufuku vyakula hivyo vya kisasa mbali na kuwafukuza wachezaji walionenepa katika mazoezi ya kikosi chake.

Clichy amesema wamekatazwa kula Pizza, baadhi ya sharutabi (Juice) na vyakula vingine vyenye mafuta mengi.

”Endapo umenenepa hautajiunga na timu katika mazoezi”

”Ikiwa uzito wako wa kawaida ni takriban kilo 60 na ukapatikana umepitiliza kilo 70 fahamu kuwa utapigwa marufuku hadi pale utakapopunguza uzito.”

”Kwa kweli hii ndiyo mara ya kwanza kabisa kwa meneja kudhibiti uzani wa wachezaji .”

”Ni jambo la kufurahia, inakupa nadharia ya klabu inayoendeshwa kitaaluma” Mchezaji huyo raia wa Ufaransa alielezea.

 

Tayari wachezaji kadhaa wamepigwa marufuku kujiunga na kikosi cha Man Utd ambacho kipo nchini China kikijiandaa na msimu mpya wa ligi kuu ya soka nchini England.

Kikosi cha Man City kesho kitapambana na Borussia Dortmund katika michuano wa kimataifa wa klabu bingwa (ICC) huko nchini China.

Mchezo wa awali wa kirafiki kwa Man City ambao ulipaswa kuwakutanisha dhidi ya mashasimu wao Man Utd, ulifutwa baada ya mvua kubwa kunyesha mjini Beijing nchini China mwanzoni mwa juma hili.

 

Video: Baraza la sanaa Tanzania lamfungia Nay wa Mitego
Sheria Ya Wachezaji Wanne Wa Akiba Kutumika England