Elizabeth Michael baada ya kufanya vizuri na filamu yake ya Mapenzi ya mungu  ambayo ilimpatia tuzo za Afrika Magic ameamua kuvunja ukimya kwa filamu mpya itakayo kwenda kwa jina la Ni noma.

ni-noma-cut

Lulu amesema mapinduzi katika filamu hiyo yataonekana kwa kuwa baadhi ya sauti zimefanyika studio ili kuhakikisha sauti zinapatikana kwa uzora zaidi pamoja vitu vingine ndio sababu ya kukaa kimya mda mrefu ili kujua mashabiki wanahitaji nini na kitu gani kwenye tasnia kimekosekana.

“Tumejitahidi kufanya production ya tofauti ambayo ina quality nzuri, it needs time, sio kama zamani kwa siku mnaweza mkashoot scene sita, saba, lakini saa zingine production kwa siku tulikuwa tunaweza kushoot scene mbili tu lakini mnahakikisha mnatoka na kitu kizuri, Lulu aliiambia bongo5

Aidha amesema kuwa katika filamu hiyo wametumia watu wengi wapya lakini ambao wana uwezo wa kufanya vizuri huku muongozaji wa filamu hiyo akitajwa kuwa ni Karabani.

Lulu amesema filamu hiyo itapatikana katika App ya proin box  ambapo anahitaji kufanya mapinduzi katika usambazaji wa filamu tanzania kwa kueleza mpango wake wa kuwafikia mashabiki wake wote wa nchi nzima

Lulu amesema watu wataweza kununua filamu hiyo kwenye app ya Proin Box kwa 2500 kwa kupitia huduma za malipo ya simu kama M-Pesa, Airtel Money na zingine huku wale waliopo nje ya nchi wakiweza kununua kwa credit cards na baadae kabisa itapatikana kwenye DVD ambayo kutakuwa na vitu vya ziada kama vile behind the scenes, interview na vitu vingine.

Ameongeza kwamba ni noma ni filamu ambayo inamzungumzia mwanamkea anayeishi maisha yasiyo na uhalisia huku akitumia uzuri wake kama ngao ya kumfanya aishi maisha mazuri na kusema ijumaa hii apa ya tar 15 inatarajiwa kuachiwa.

 

Adidas Waipandisha Man Utd Viwango Vya Utajiri Dunaini
Video: Ni Noma ya Lulu Kuingia Sokoni Rasmi