Mabingwa wa soka barani Ulaya, klabu ya  Real Madrid usiku wa kuamkia hii leo walitwaa ubingwa wa kombe la Uefa Super cup kwa kuilaza Sevilla CF kwa mara nyingine tena.

Real Madrid waliibuka na ushindi wa mabao 3-2 huku bao la ushindi la Dani Carvajal likifungwa dakika 11 kabla ya dakika 120 kuhitimishwa.

Katika mchezo uliochezwa kwenye uwanja Lerkandal, Sergio Ramos aliwaokoa Real kwa kufunga bao la kusawazisha sekunde chache kabla ya kipenga cha dakika tisini kupulizwa na kuupeleka mchezo katika muda wa ziada.

Real Madrid walianza pambano vizuri na kufanikiwa kupata bao la uongozi kuipitia kwa chipukizi Marco Asensio.

Sevilla walisawazisha dakika chache kabla ya mapumziko kupitia kwa Franco Vazquez.

Zikiwa zimebakia dakika 18 pambano kumalizika, Yevhen Konoplyanka aliifungia penati Sevilla baada ya Ramos kumuangusha Vitolo.

Ramos alijivua lawama kwa kuisawazishia Real bao la pili sekunde chache kabla ya kipenga cha muda wa kawaida kupulizwa ndipo na kupelekea dakika 30 za muda wa ziada kuongezwa.

Lissu adai kushtukia njama za kuwavua ubunge yeye na Mbowe
Naibu Waziri Wa Ujenzi Mhandisi Ngonyani Akanusha Tuhuma Za Kumchafua Raisi Magufuli