Wakati michezo ya Olimipiki 2016 inayofanyika Rio, Brazil ikiendelea kushika kasi na rekodi zikiendelea kuwekwa kwa wanamichezo zaidi ya 11,000 ambao wameshiriki mashindano ya mwaka huu, mwanariadha kutoka Jamaica, Usain Bolt ameweka historia ya kipekee katika michezo hiyo.

Katika mbio za mita 100, Bolt ameibuka mshindi kwa kutumia sekunde 9.81 na kushinda medali ya dhahabu, nafasi ya pili ikishikwa na Justin Gatlin kutoka Marekani akitumia sekunde 9.89 na kushinda medali ya fedha na nafasi ya tatu Mcanada, Andre de Grasse akitumia sekunde 9.91 na kushinda medali ya shaba.

Pamoja na ushindi huo, Usain Bolt amekuwa mwanamichezo wa kwanza kushinda medali za dhahabu mara tatu katika michezo ya Olimpiki, akianzia Beijing, China 2008, London, Uingereza 2012 na mwaka huu 2016 Rio, Brazil.

UVCCM waanza kutumbuana
CUF yampiga chini rasmi Profesa Lipumba