Meneja wa klabu ya Real Madrid, Rafa Benitez ametangaza uhakika wa kuendelea kufanya kazi na beki wa kati Sergio Ramos ambaye anatajwa kuwa katika mipango ya kusajiliwa na mashetani wekundu, Manchester United.
Benitez, amesema tetesi zinazo muhusu beki huyo kuelekea Man utd hazipi nafasi kichwani mwake kutokana na kuamini kwamba ni sehemu ya kazi ya vyombo vya habari ni kuandika taarifa zinazokwenda kwa umma lakini anavyofahamu yeye bado Ramos ataendelea kuwa katika himaya yake.

Meneja huyo aliyekabidhiwa jukumu la kukiongoza kikosi cha Real Madrid miezi miwiwli iliyopita, amesema ana mahusiano mazuri na Ramos na haoni tofauti zinazoripotiwa katika baadhi ya vyombo vya habari ambazo zinatajwa kuwa kikwazo kwa beki huyo kuendelea kubaki klabuni hapo.

Hata hivyo Benitez amemuomba meneja wa klabu ya Man Utd, Louis Van Gaal kuachana na mipango ya kumfuatilia beki huyo mwenye umri wa miaka 29, kutokana na kuamini kwamba kinachofanyika kwa sasa ni sawa na kazi bure.

Man Utd wanaamini wanaweza kumpata kwa urahisi Sergio Ramos, kwa mtego wa mlinda mlango wao David De Gea ambaye anaonekana kuhitajika kwa udi na uvumba huko Estadio Santiago Bernabeu kama mbadala wa Iker Cassillas aliyetimikia FC Porto.

Tanzia: Mtoto Wa Whitney Houston, Bobbi Kristina Afariki
AS Monaco Wakubali Yaishe Kwa Moutinho