Meneja wa klabu ya Stoke City, Mark Hughes amepangua tuhuma zinazomuandama mshambuliaji wake mpya Xherdan Shaqiri, ambaye alijiunga na The Potters mwanzoni mwa juma hili akitokea Inter Milan ya nchini Italia.

Shaqiri, anatuhumiwa kutanguliza maslahi ya pesa zaidi na kusahau umuhimu wa soka lake, ambao ulikua unahitajika kwenye klabu zinazocheza michuano mikubwa barani Ulaya.

Tuhuma kwa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 23, zilitolewa na gwiji wa soka nchini Ujerumani, Stefan Effenberg ambaye alionyesha kushangazwa na maamuzi ya Shaqiri ya kuikataa ofa ya klabu ya Schalke 04 inayoshiriki ligi ya Bundesliga.

Hughes, amesema tuhuma zinazoelekezwa kwa Shaqiri hazina ukweli wowote zaidi ya kuamini kuna baadhi ya watu wamechukizwa na maamuzi yaliyochukuliwa na mshambuliaji huyo, ambaye aliwahi kucheza soka nchini Ujerumani akiwa na mabingwa FC Byern Munich.

Hughes, alipangua tuhuma hizo alipokua kwenye mkutano na waandishi wa habari, kwa kuambatana na Shaqiri, kwa ajili ya kuzungumzia mchezo ujao wa ligi kuu ya soka nchini England ambapo Stoke City watapapatuana Tottenham Hotspurs.

                                                                                                                                                 Stefan Effenberg

Effenberg anaamini Shaqiri, alikua na nafasi ya kipekee ya kucheza kwenye klabu kubwa kama Schalke 04, ambayo amekiri hailingani na Stoke City na pia klabu hiyo ya Veltins-Arena, Gelsenkirchen itashiriki michuano ya Europa league.

Xherdan Shaqiri, tayari ameshasaini mkataba wa miaka mitano wa kuitumikia Stoke City ambayo imemsajili kwa ada ya paund million 12.

Baines Nje Majuma 12-13
Arsenal Wapata Ahuweni