Ligi Kuu ya Vodacom mzunguko wa 15 unatarajiwa kuendelea kesho Jumatano kwa michezo mitano, na Alhamisi kwa michezo mitatu kwa kila timu kusaka pointi tatu muhimu katika mzunguko huo.

Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, Maafande wa JKT Ruvu watawakaribisha Simba SC, Ndanda FC watakua wenyeji wa Mbeya City kwenye uwanja wa Nangwanda Sijaona.

Tanzania Prisons watakua wenyeji wa Coastal Union katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, Stand United watacheza dhidi ya Toto Africans kwenye uwanja wa Kambarage, huku Mgambo Shooting wakiwakaribisha Azam FC kwenye uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.

Alhamisi ligi hiyo itaendelea kwa michezo mitatu, Mwadui FC watawakaribisha Kagera Sugar katika uwanja wa Mwadui, African Sports watakua wenyeji wa Mtibwa Sugar uwanja wa Mkwakwani jijini Tnaga, huku Young Africans wakiwakaribisha Majimaji FC katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Rais Wa Soka La Barani Asia Atembelea Wizarani
Snoop Dogg awaporomoshea matusi waandaaji wa tuzo za Oscar