Cardi B ni msanii wa kike anayefanya muziki wa hip hop ambaye anatamba kwa ngoma yake inayoitwa ‘Bodak Yellow’ ambayo kwa sasa inashika namba moja katika chati za Billboard Hot 100, msanii huyo anagonga vichwa vya habari mbalimbali kwa sasa katika tasnia ya muziki wa hiphop kutokana na ngoma yake kuwa na mafanikio makubwa.

Wasanii mbalimbali wamekuwa wakimtumia pongezi rapa huyo baada ya wimbo wake kushika namba moja na miongoni mwa watu waliompongeza ni rapa Nick Minaj ambaye kupitia ukurasa wake wa Twitter Nick Minaj amempogeza Cardi B kwa kupata mafanikio hayo.

Cardi B amekuwa msanii wa kwanza wa kike wa Hip hop kufika namba moja katika chati za Billboard Hot 100 tangu alipofanya hivyo msanii Lauryn Hill miaka 19 iliyopita.

Congratulations to a fellow NEW YAWKA on a RECORD BREAKING achievement. Bardi, this is the only thing that matters!!! Enjoy it??? @iamcardib

— NICKI MINAJ (@NICKIMINAJ) September 25, 2017

Baada ya ujio wa Cardi B na mafanikio yake watu wengi walifikiri kwamba Nick Minaji asingependa kinachotokea kwani wamekuwa wamshindanisha na wasanii wakike wa hip hop wapya wanaoibuka na kujaribu kumpa changamoto.

Ikumbukwe kwamba pamoja na mafanikio ya Nick Minaj, hajawahi kuwa na wimbo uliofika namba moja katika chati ya Billboard Hot 100 ingwa yeye ndiye msanii pekee wa kike aliyeingiza nyingi katika chati hizo akiwa ameingiza nyimbo 76.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter Cardi B alipost ujumbe akimshkuru Nick Minaj kwa kuonyesha mapenzi kwake na kumpongeza.

Thank you!! This means sooo much coming from you!! ❤️ https://t.co/vPGwFiBAiQ

— iamcardib (@iamcardib) September 25, 2017

Mwigulu awatumia salamu ‘watu wasiojulikana’, akataa ya Chadema
Marekani 'yanawa mikono' vita na Korea Kaskazini, ndege zake kuwindwa