Card B afunguka kuhusiana na sakata la kumvamia ‘rapper’ mwenzake Nick minaj na kutaka kuzichapa  kwenye sherehe ya ‘Harper’s Bazaar’ New York usiku wa Septemba 7, 2018

‘W Magazine’ imefanya mahojiano na Card B ameeleza na kusema kuwa aliwahi kuzungumza na Nicki minaj mara mbili na waliyamaliza lakini Nick minaj kwa upande wake ameendelea kumuongelea vibaya  katika mitandao ya kijamii.

Aidha ameeleza kuwa kitu ambacho kimemuumiza zaidi Cardi B ni ‘like’ ya Nicki minaj kwenye mtandao wa twitter iliyopostiwa na mashabiki  inayosema kuwa hajui kumlea mtoto wake Kulture na alishangazwa na like hiyo kutoka kwa Nick minaji  kwani hana hata mtoto na hajui malezi ya watoto.

Ameongeza kuwa “Kwa muda sasa Nick minaj amekuwa akinirushia maneno na niliongea nae kama mara mbili na tukaelewana, lakini aliendelea na maneno ya kejeri.  Card B amesema ‘ mimi ni mama mzuri na najua kulea”.

Hata hivyo Nicki Minaj aliwahi kukanusha kuhusiana na taarifa hizo za kumkejeri rapper mwenzake  kupitia radio yake ya “Queen’s Radio” na kusema kuwa  ‘’ hajawahi kumuongelea mtoto wa mtu yeyote vibaya na wala kuongelea kuhusu matunzo  ya mtoto yeyote.

 

Majaliwa amtaka DC Shekimweri kufanya uchunguzi
Baada ya kustaafu John Terry kumsaidia Dan Smith