First Lady wa Young Money, Nicki Minaj ametengeneza rasmi uadui na Miley Cyrus baada ya kumponda wakati anapokea tuzo ya video bora ya hip hop (Anaconda) kwenye jukwaa la MTV/VMAs 2015, Jumapili, Agosti 30.

Nicki alimrushia maneno Miley Cyrus ambaye alikuwa mshereheshaji katika tuzo hizo ikiwa ni majibu yake kwa Miley aliyetoa maoni juu ya bifu la rapa huyo wa kike na Tailor Swift hivi karibuni alipofanya mahojiano na The New York Times akidai kuwa majibu ya Nicki kwa Swift hayakuwa ya upole na ukarimu.

Akiwa jukwaani, Nicki alianza kwa kuwashukuru mashabiki wake kwa kumuwezesha kushinda tuzo hiyo na mwisho akamjibu Miley kwa kumtaja jina huku akitumia maneno makali.

“Back to this b***h that had a lot to say about me the other day in the press. Miley, what’s good?,” aliuliza Nicki na kuwaacha watu midomo wazi.

Miley naye alirukia na kujibu haraka akidai vyombo vya habari vinapika mambo huku akimpongeza Nicki kwa ushindi wake kama ishara ya kuua kiaina kinachoendelea.

“Hey, we’re all in this industry, we all do interviews and we all know how they manipulate s**t. Nicki, congratulations,” alijibu Miley Cyrus.

Kanye West Atangaza Kugombea Urais Wa Marekani
Tailor Swift Afunika Tuzo Za MTV/VMAs, Orodha Kamili Ya Washindi Hii Hapa