Aliyekua mshambuliaji wa klabu ya Arsenal Nicklas Bendtner anatarajia kwenda kutumikia kifungo jela kwa muda wa siku 50 kwa kosa la kumshambulia dereva Taxi.
Mshambuliaji huyo kutoka nchini Denmark anayecheza ligi ya Norway katika klabu ya Rosenborg ataenda jela baada ya kuifuta rufaa yake aliyoikata baada ya hukumu kutoka mapema mwezi huu.
Hata hivyo Bendtner mwenye umri wa miaka 30, bado haijaeleweka ni lini ataanza kutumia kifungo hicho.
Bendtner ampiga na kumvunja taya ya dereva huyo mwezi Septemba mwaka huu mjini Copenhagen na mahakama ilithibitishiwa tukio hilo kwa video ya tukio hilo kutoka ndani ya taxi.
Bendtner alikataa kumlipa dereva nauli ya Pauni 4.8 ( Tsh 14,000) na baadae kuanza kumpiga, kabla ya kuendelea kumpiga akiwa amedondoka chini.
Bendtner alikiri kumpiga dereva huyo, ingawa alidai alikuwa anajilinda “Nilikabiliana nae kwa kujilinda” Mchezaji huyo alisema mahakamani.
“Nilidhani dereva angeweza kuniumiza. Kwani tulikuwa tunagombana. Tuliinua mikono yetu kwa pamoja, na mimi ndiye niliyewahi kumpiga “
Mahakama pia ilimtaka Bendtner kumlipa dereva huyo pauni 1000 ( Milioni 2.9) kama fidia, lakini mshambuliaji huyo tayari ameshaomba radhi mbele ya waandishi wa habari.
Bendtner akiomba msamaha alisema : “Nilihusika katika tukio hili la bahati mbaya. Sikufahamu litafikia kama hivi, na ni kweli nina huzuni kubwa kwamba matokeo yake yamekuwa ya bahati mbaya kama nilivyofanya.”