Klabu ya Singida Big Stars imeendelea kujiimarisha kwenye eneo lake la ulinzi baada ya kudaiwa kukamilisha usajili wa beki wa kulia Nicolas Wadada anayecheza katika kikosi cha Ihefu.

Huu ni usajili wa pili kwa Singida Big Stars baada ya kukamilisha usajili wa Yahya Mbegu ambaye waliipokonya Simba tonge mdomoni.

Habari kutoka Singida zinaeleza kuwa Wadada tayari ameshamalizana na mabosi wa Singida BS na kilichobaki anasubili dirisha la usajili lifunguliwe na atangazwe.

Inadaiwa mabosi wa Singida wanataka eneo la beki ya kulia kuwe na uzoefu kwani tayari ilishamtoa kwa mkopo Juma Abdul kwenda Kitayosce kabaki Paul Godfrey ambaye na yeye hapati nafasi ya kucheza mbele ya Nicolas Gyan.

Kuingia kwa Wadada kutatoa mwanga kwa benchi la ufundi la Singida kwani eneo hilo tayari kutakuwa na wa chezaji wawili ambao wana kiwango kizuri na kikubwa wakiwa wanaenda kimataifa.

Afisa habari wa Singida BS, Hussein Masanza alipoulizwa juu ya usajili wa Wadada amesema kwa kifupi, “Tusubiri hadi Ligi imalizike kila kitu kitakuwa wazi, kwa sasa Wadada ni mchezaji wa Ihefu kwa hiyo siwezi kuzungumzia sana.”

Chalamila, Mwasa wakabidhiana ofisi Kagera
Angola yawa nchi Mwanachama wa 21 wa ATI