Mabingwa wa Soka nchini England Manchester City wamepanga kufanya kufuru kwa kutoa zaidi ya Pauni 103 milioni kumsajili kiungo wa Inter Milan, Nicolo Barella mwenye umri wa miaka 26, katika dirisha hili ikiwa Benardo Silva ataondoka kujiunga na Paris St-Ger-main.

Hadi sasa hakuna muafaka uliofikiwa juu ya hatma ya Silva ingawa taarifa za ndani zinadai staa huyo ameomba kuondoka ili kupata changamoto mpya sehemu nyingine, na mbali ya ofa za Saudi Arabia, PSG pia imeonyesha nia ya kutaka kumsajili.

Mpunga huo ambao Man City imepanga kuutoa huenda ukazidi, kwa sababu Liverpool pia inamuangalia fundi huyu kama mbadala wa Jordan Henderson ambaye anatarajiwa kukamilisha uhamisho wake wa kutua Saudi Arabia katika siku chache zijazo.

Barella ambaye mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2026, msimu uliopita alionyesha kiwango bora hususani kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa ambako aliiwezesha Inter kufika fainali ingawa ilipoteza mbele ya Man City.

Namungo FC yasajili mshambuliaji mzoefu
Mrithi wa Mkude arusha dogo kwa jirani