Mwanaume aliyewaua wanawake tisa katika hoteli mbalimbali nchini Nigeria na kesi yake kuibua ghadhabu amehukumiwa kunyongwa katika mji wa Port Harcourt.

Waendesha mashtaka wamesema mwanaume huyo, mwenye miaka 26, Gracious David-West aliwanyonga wanawake hao aliokuwa anakutana nao katika hoteli mbalimbali nchini humo kati ya mwezi Julai na Septemba 2019

Wakati wa mfululizo wa mauaji ya wanawake hao mwezi Septemba mwaka jana, raia wenye hasira waliandamana barabarani na kuitaka mamlaka kuchukua hatua kutatua tatizo hilo.

Mtuhumiwa huyo alikamatwa Septemba 19, wakati akijaribu kuondoka Port Harcourt ambapo mamlaka ilikuwa karibu kumkuta na hatia.

Picha za video za CCTV zilimuonesha akiwa anaondoka hotelini na picha hizo zilienea katika mitandao ya kijamii.

Polisi wanasema David-West alikuwa mjumbe wa kikundi cha wanamgambo wa kigaidi kijulikanacho kama Greenlanders – au Dey Gbam.

Jaji Adolphus Enebeli amesema kifo chake kitatekelezwa kwa kunyongwa.

Hukumu hiyo ya kifo ni nadra sana kutolewa nchini Nigeria na mara ya mwisho kutolewa ilikuwa ni mwaka 2016 kwa watu watatu.

Wizara ya maji yaagiza Bukoba mjini kufikishiwa maji kwa asilimia 100
TCU yafungua awamu ya pili ya udahili