Afisa mkuu wa afya katika taasisi ya kukabiliana na maradhi ya kuambukiza barani Afrika John Nkengasong amesema aina nyingine mpya ya kirusi cha corona imejitokeza nchini Nigeria. 

Nkengasong ameeleza hayo leo alipozungumza na waandishi wa habari ambapo amesema kuwa kirusi hicho ni tofauti na vile vilivyogunduliwa Uingereza na Afrika Kusini lakini uchunguzi zaidi unahitajika. 

Ameongeza kuwa taasisi ya Nigeria ya kukabili magonjwa ya kuambukiza pamoja na taasisi ya Afrika kuhusu maradhi hayo, zinachunguza sampuli kadhaa za kirusi hicho. 

Tahadhari hiyo imejiri wakati wakati huu kukiwa kuna ongezeko la maambukizi ya virusi vya corona katika bara la Afrika.

Barani Ulaya nako ambako hadi sasa kumeripotiwa zaidi ya visa Milioni 20, Wiki iliyopita Uingereza iliripoti aina mpya ya virusi vya Corona.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Desemba 26, 2020
Ethiopia: Watu 100 wauawa, Abiy atuma wanajeshi

Comments

comments