Kampuni ya vifaa vye michezo ya Nike imezindua rasmi mipira itakayotumika kwenye ligi za nchini Uingereza, Italia pamoja na Hispania kwa msimu wa 2015-16.

Kampuni ya Nike inayodhamini ligi hizo upande wa vifaa, imezindua mipira hiyo kwa kutoa picha ambazo zinaonyesha utofauti uliopo kwa kuzingatia rangi ambazo zitatumika.

Ligi ya Uingereza ambayo ni maarufu sana duniani itatumia mpira ulionakshiwa rangi ya nyekundu kwa kiasi kikubwa na ligi ya nchini Hispania utatumia mpira wenye asilimia kubwa ya rangi ya ‘pink’ huku ligi ya nchini Italia itakuwa na mpira ulionakshiwa rangi ya kijani mpauko.

Hata hivyo mipira hiyo mitatu imetengeneza kwa malighafi moja ikitofautishwa kwa rangi tu.

Matola Ataja Waliopendekeza Usajili Wa Kiiza Simba
Argentina Kiboko, Yaifuata Chile Fainali Kwa Kipigo Kitakatifu