Rapa Nikki Mbishi ametangaza rasmi kuwa album yake mpya ‘Welcome to Gamboshi’ tayari imefikia asilimia takribani 97 kukamilika ili kuwa tayari kuingia sokoni.

Nikki Mbishi amewataarifu mashabiki wake kupitia mfululizo wa maandiko kadhaa kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Instagram huku akidokeza kuwa ujio wa album hiyo utaambatana na bidhaa kadhaa kutoka kwake ikiwamo mavazi.

“Mpaka sasa Welcome to Gamboshi Album imefikia asilimia 97,” ameandika Nikki.

Album hiyo ina jumla ya nyimbo 23 huku rapa huyo akiwa ameshirikiana na wasanii mbali mbali, akiwamo Ally Choki, PMawenge, Wakazi, Tk Ndendezi, Zaiid pamoja na wengine wengi.

Google yasitisha mapato ya matangazo kwa vyombo vya habari Urusi
Baraza kuu la Umoja wa mataifa kujadili Ukraine kwa dharura leo