Msanii wa muziki wa hiphop, mwanazuoni na mmoja wa waanzilishi wa kampuni ya weusi na taaisi ya maendeleo ya jamii twaonekana, Nikki wa pili, ni moja kati ya waandishi wazuri wa mashairi na wenye upeo mkubwa kifikra ambao kupitia kurasa zao za mitandao ya kijamii hutumia kuelimisha jamii kwa kuandika jumbe zenye ukweli na zinazogusa maisha ya watu moja kwa moja.
Leo katika ukurasa wake wa instagram ameandika hivi;
”Bibi zetu walikuwa wana amkia shambani asubuhi, wanalima kwa jembe la mkono wanakatia ng’ombe majani, wanaenda kuchota maji mbali, wanafua, jioni wana kamua maziwa na bado walikuwa wanapikia baba zetu, sasa msichana anaenda kazini na gari, kazini kiyoyozi, kiti cha kuzunguka, lakini akirudi nyumbani anasema kachoka hawezi kupika”.
-
Video: Diamond akionesha vifaa vya gharama vya Wasafi radio na Wasafi TV
-
Video: Linah aja na ”Same boy” kama ya R-Kelly na Usher ”same girl”
Amesema Kabla hatuja andesha ndoa zetu kizungu, tukumbuke huko kwao talaka 60% yani zimewashinda, na kabla ya kudharau utaratibu wa wazee wetu, tukumbuke kuwa babu na bibi zetu wamezeeka pamoja amemalizia hivyo.
Katika moja ya mahojiano Nikki ameeleza kuwa mahusiano mazuri kati ya baba na mama yanamchango mkubwa sana kwa malezi na makuzi ya watoto.
Hivyo amesisitiza na kushauri kuwa Upendo wa baba kwa mtoto usizidi upendo wa baba kwa mke wake na upendo wa mama kwa mtoto usizidi upendo wa mama kwa mume wake, kwani makuzi ya mtoto hutegemea mahusiano mazuri kati ya mama na baba au mke na mume.